Vichwa Vya Habari
Language
Saturday, 9 February 2013
MICHEZO: HIVI NDIVYO DROGBA ALIVYO POKELEWA UTURUKI
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Ivory Coast, Didier Drogba amepata mapokezi mazuri alipowasili Istanbul
alipokubali kujiunga na Galatasaray ya Uturuki katika uhamisho wa Januari.
Kiungo wa
zamani wa Inter Milan, Wesley Sneijder alipata mapokezi kama hayo alipowasili
Uturuki mwezi uliopita na Drogba ameamua kumfuata Mholanzi huyo akiondoka
Shanghai Shenhua ya China.
Nahodha
huyo wa Ivory Coast alichelewa kuwasili kwenye timu hiyo kwa sababu ya Fainali
za Mataifa ya Afrika.

Mshambuliaji
mwingine wa zamani wa Chelsea, ambaye alitoka Stamford Bridge kwenda China,
Nicolas Anelka amerejea Ulaya.
Nicolas
Anelka alijiunga na Shenhua Januari mwaka jana, lakini ameamua kujiunga na
vigogo wa Italia, Juventus, akikamilisha uhamisho wake kwa mabingwa hao wa
Serie A mwezi uliopita.
MICHEZO: MESSI ASAINI MKATABA MPYA BARCA MPAKA 2018
MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amesaini mkataba mpya na Barcelona,
ambao utamfanya aichezee klabu hiyo hadi Juni 30 mwaka 2018, vinara hao wa Ligi
Kuu ya Hispania.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25, amesaini mkataba ambao alifikia makubaliano
Desemba, mwaka jana ambao unahusisha pia miaka miwili aliyobakiza katika
mkataba wake wa sasa na atapiga kazi Nou Camp hadi akiwa na miaka 31.
HABARI MUHIMU: UFISADI WA SERIKALI WAANIKWA BUNGENI

Ripoti ya Kamati Maalumu ya Spika, kuhusu vyanzo vya mapato ya
HABARI MUHIMU: KAMATI YA ZITTO KABWE YATUPWA KAPUNI

Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za
POAC sasa zitaendelea kufanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),
ambayo itaendelea na jukumu lake la msingi la kuchambua taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kwa Serikaki
Kuu.
Kamati nyingine iliyofutwa ni ya sheria ndogo,
huku Spika akiunda kamati mpya tatu na nyingine kuzifanyia marekebisho
kadhaa ikiwa ni hatua ya kuimarisha usimamizi wa Bunge kwa shughuli za
Serikali.
Akitangaza mabadiliko hayo muda mfupi kabla ya
kuahirisha mkutano wa kumi jana, Makinda alizitaja kamati mpya kuwa ni
Kamati ya Bajeti, Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama, ambayo imetenganishwa kutoka Kamati ya
kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Kwa mujibu wa Spika Makinda majukumu ya kamati
mpya ya bajeti ni kufuatalia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, Sera za
Fedha, kuanisha na kupendekeza vyanzo vya mapato ya Serikali na
kufuatilia mwenendo wa uchumi.
Kamati hiyo pia imepewa jukumu la kushauri kamati nyingine zote kuhusu bajeti.
“Kwa sasa kuna baadhi ya kamati zinazosimamia wizara moja moja, ambazo shughuli zake siyo nyingi ikilinganishwa na kamati nyingine zinazosimamia wizara zaidi ya moja zikiwa na shughuli nyingi,”alisema Makinda na kuongeza:

“Vivyo hivyo kuna wizara zinazohusika na
kutunga sera, lakini kwa kiasi kikubwa sera hizo zinatekelezwa na wizara
nyingine hadi ngazi za chini. Mfumo huu husababisha baadhi ya Kamati za
Bunge kutoweza kufuatilia vizuri utekelezaji wa shughuli za Serikali,
kinyume na matakwa ya ibara ya 63(3) ya Katiba na majukumu ya kamati
yaliyoainishwa na Kanuni za Bunge.”
Spika alifanya marekebisho hayo kwa mamlaka aliyopewa kwa kanuni ya 152 (3) cha Kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2007.
Kamati ambazo zimebadilishwa miundo yake ni ya Katiba, Sheria na Utawala, Fedha na Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya Ukimwi.
Kamati ambazo zimebadilishwa miundo yake ni ya Katiba, Sheria na Utawala, Fedha na Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya Ukimwi.
Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara imeundwa
na imepewa wajibu wa kusimamia masuala ya uchumi, mitaji, uwekezaji,
maendeleo ya viwanda na shughuli za biashara.
Makinda alisema Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, imepunguziwa majukumu na sasa itajikita kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na taasisi zake na Wizara ya Katiba na Sheria.
“Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itasimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), pamoja na sheria ndogo za halmashauri zote nchini,”alisema Makinda.
Alisema kwamba jukumu la Kamati ya Huduma za Jamii ni kufuatilia utekelezaji wa Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi kwa ngazi ya elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu, Elimu ya Ufundi (Veta) na taasisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Pia Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma, Baraza la
Mitihani, Taasisi ya Kukuza Mitaala na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Kamati hiyo pia itasimamia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati Nyingine ni ya Ukimwi na Dawa za kulevya, ambayo imeongezewa jukumu la kufuatilia masuala ya matumizi ya dawa hizo.
Spika alilieleza Bunge kuwa Kamati Nyingine ni ya Ukimwi na Dawa za kulevya, ambayo imeongezewa jukumu la kufuatilia masuala ya matumizi ya dawa hizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)