WAKATI Watanzania wakianza kusahau msiba wa kuanguka kwa jengo lenye
ghorofa 16 Machi 29, mwaka huu jijini Dar, imegundulika kati ya watu 36
waliofariki dunia kutokana na ajali hiyo, yumo msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Gabriel Godwin Kimwela.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Mboka Godwin, Gabriel alikuwa akifanya shughuli za ujenzi katika jengo hilo lililopo kati ya Mtaa wa Indira Ghandhi na Barabara ya Morogoro na alifariki mara baada ya jengo hilo kuanguka.
“Maiti tuliisafirisha na kuipeleka Mbeya,” alisema Mboka na kuongeza kuwa mbali na kuwa msanii, kaka yake aliwahi kujihusisha na siasa kwa kuwapigia debe wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na John Mnyika katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika sanaa, Gabriel aliwahi kutoa albamu moja kwa ufadhili wa shirika moja la Kimarekani iliyorekodiwa katika ya Zinji Record.
Nyimbo zake zilizopata kusikika redioni ni Africulture na Tumeshachoka. Mwaka 2004, Gabriel alianzisha Kundi la Wakubwa Family ambalo baadhi ya wasanii wake wanajipanga kumtungia wimbo wa kumuenzi wakimshirikisha Z-Anto.
No comments:
Post a Comment