Kwa kutumia mabango, lengo likiwa kutangaza kazi zao, waganga
wengi wa tiba asilia wamekuwa wakijinadi kuwa wanatoa tiba ya kurefusha
maumbile ya siri ya wanaume, kukuza makalio au matiti.
Katika mitaa ya miji na majiji nchini, siyo jambo
la ajabu kukutana na mabango hayo, ambayo hata hivyo kushamiri kwake
kunaleta picha kwamba ni kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo
nchini, huku watoa huduma husika wakinufaika kwa kujikusanyia kiasi
kikubwa cha fedha kutoka kwa wahitaji.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama
‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa
ubora na kwamba zina madhara makubwa.
Lakini, sasa unaweza kuachana na dawa hizo za
Kichina, baada ya kugundulika mmea wenye uwezo wa kukuza makalio,
matiti, pamoja na kurefusha