MNAMO TAREHE 08.02.2013 MAJIRA YA SAA
06:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI KATA YA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL
S/O MWASALEMBA,MIAKA 18,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA ITIJI ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA
KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA PETER
Vichwa Vya Habari
Language
Friday, 8 February 2013
MICHEZO: VPL KESHO INAINGIA RAUNDI YA PILI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa
2012/2013 inaingia raundi ya 16 kesho (Februari 9 mwaka huu) kwa mechi
nne ambapo Oljoro JKT itaikaribisha Simba jijini Arusha.
Mechi hiyo namba 129 itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 tu utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mgambo Shooting. Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Amon Paul kutoka Musoma mkoani Mara.
Toto Africans baada ya kufanya vibaya katika mechi
HABARI MUHIMU: MAPENZI YAUA MMOJA KILIMANJARO
WATU wawili wamefariki dunia katika
matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu kujinyonga kwa
kutumia kipande cha kanga.
Katika
tukio la kwanza mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Aloyce Msabaha (58), mkazi
wa Kibosho Kitandu, Moshi Vijijini alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia
kipande cha kanga na kuacha ujumbe mzito kuhusiana na kifo chake.
Shuhuda wa
tukio hilo, aliyefahamika kwa jina la Msabaha ambaye ni baba wa familia ya mke
na watoto haifahamiki ilikuwaje mpaka akafikia hatua ya kusitisha uhai wake
japo taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai ni wivu wa mapenzi.
Hata hivyo Shuhuda huyo amesema waulikuta mwili wa marehemu
HABARI MUHIMU: TV 'RUNINGA' HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME!!!
WANAUME wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama
runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama
runinga mara chache.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.
Imeelezwa kuwa wanaume wanaotazama runinga kwa
zaidi ya saa 20 kila wiki wanapoteza asilimia 44 ya mbegu za kiume
ukilinganisha na wale wasiotumia muda mrefu katika runinga.
HABARI MUHIMU: BAADA YA ARVs FEKI, HOFU YA DAWA FEKI ZA TB YATANDA TZ
DAWA bandia zinazodaiwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB),
zinahofiwa kuingia nchini, ambapo zinadaiwa kutumika kwa kipindi cha
zaidi ya miaka miwili tangu mwaka 2011.
Dawa hizo zinazodaiwa kusambaa katika miji mikubwa
ya Afrika, zinadaiwa kuanza kuleta madhara kwa watumiaji kwani hazina
uwezo wa kuua wadudu wanaosababisha ugonjwa huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)