WANAUME wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama
runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama
runinga mara chache.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.
Imeelezwa kuwa wanaume wanaotazama runinga kwa
zaidi ya saa 20 kila wiki wanapoteza asilimia 44 ya mbegu za kiume
ukilinganisha na wale wasiotumia muda mrefu katika runinga.
Vilevile, wanaume wanaofanya mazoezi kwa zaidi
ya saa 15 kwa wiki, wana uwezo wa kuongeza asilimia 73 ya mbegu zao
ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi au wanaofanya mazoezi chini ya
saa tano kwa wiki.
Kiongozi wa utafiti huo, Dk Audrey Gaskin
alisema mtindo wa maisha unachochea zaidi upungufu wa mbegu za kiume na
uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Mtafiti huyo alifanya uchunguzi wa viwango vya
mbegu za kiume za wanaume 189 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 22
kuanzia mwaka 2009 hadi 2010.
Wanaume hao walihojiwa kuhusu kiwango cha
ufanyaji wao wa mazoezi, muda wanaotumia katika kutazama runinga au
filamu katika kipindi cha miezi mitatu.
“Baada ya utafiti huo, nusu ya wanaume
wasiofanya mazoezi na waliotumia muda mrefu katika runinga walikuwa na
kiwango hafifu cha uzalishaji wa mbegu,” alisema Dk Gaskin.
Dk Gaskin alisema: “Masuala mengine ya kiafya yanayoweza kuathiri kiwango cha mbegu za kiume ni chakula, msongo wa mawazo na uvutaji wa sigara,” alisema.
Dk Gaskin alisema: “Masuala mengine ya kiafya yanayoweza kuathiri kiwango cha mbegu za kiume ni chakula, msongo wa mawazo na uvutaji wa sigara,” alisema.
Daktari huyo alisema mwanamume anapokaa kwa
muda mrefu katika sofa mbegu za kiume zinapata kiwango kikubwa cha joto
ambalo huathiri uzalishwaji wa mbegu.
Alisema wanaume wanaohitaji watoto wanatakiwa kuacha kuvaa nguo za ndani zinazobana ili kuimarisha kiwango cha mbegu za kiume huku madereva na waendesha baiskeli wakionywa kuwa katika hatari ya kupungukiwa kutoa mbegu nyingi.
Alisema wanaume wanaohitaji watoto wanatakiwa kuacha kuvaa nguo za ndani zinazobana ili kuimarisha kiwango cha mbegu za kiume huku madereva na waendesha baiskeli wakionywa kuwa katika hatari ya kupungukiwa kutoa mbegu nyingi.
Mhadhiri Mkuu katika Chuo Kikuu cha Sheffield
nchini Uingereza, Dk Allan Pacey anasema matokeo ya utafiti wake
yatasaidia kuelimisha umma.
Hata hivyo, Daktari bingwa wa Uchunguzi wa
Magonjwa kwenye Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Muhimbili,
Henry Mwakyoma aliyewahi kufanya utafiti kuhusu ugumba kwa wanaume,
alisema bado utafiti wa Dk Gaskin una maswali mengi.
“Siwezi kuukubali au kuukataa utafiti wake,
inawezekana ni mionzi au joto ndilo linalosababisha udhaifu wa mbegu
hizo, lakini bado utafiti wake una maswali mengi,” alisema Dk Mwakyoma.
jAMANI AU NDO MANA TATIZO HILO LIMEKOMAA SANA SIKU HIZI???/DUU
ReplyDelete