WATU wawili wamefariki dunia katika
matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu kujinyonga kwa
kutumia kipande cha kanga.
Katika
tukio la kwanza mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Aloyce Msabaha (58), mkazi
wa Kibosho Kitandu, Moshi Vijijini alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia
kipande cha kanga na kuacha ujumbe mzito kuhusiana na kifo chake.
Shuhuda wa
tukio hilo, aliyefahamika kwa jina la Msabaha ambaye ni baba wa familia ya mke
na watoto haifahamiki ilikuwaje mpaka akafikia hatua ya kusitisha uhai wake
japo taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai ni wivu wa mapenzi.
Hata hivyo Shuhuda huyo amesema waulikuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia katika mti wa mwembe uani,
nyumbani kwake.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amesema,
baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, polisi walifika katika eneo la
tukio na kukuta mwili wa marehemu pamoja na karatasi kilichokuwa na ujumbe.
Tukio hilo
lilitokea majira ya saa saba usiku ambapo inadaiwa kuwa mwili wa marehemu
uligundulika asubuhi ukiwa umening’inia katika mti wa mwembe jirani na nyumba
ya marehemu.
Katika
tukio la pili, Mtembea kwa miguu, Raphael Maro (48), mkazi wa Uru Kariwa
aligongwa na pikipiki, lililokuwa likiendeshwa na mtu mmoja ambaye hakuweza
kufahamika mara moja kutokana na kukimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Kamanda
Boaz amesema tukio hilo lilitokea, Februari 5, majira ya saa 4 usiku, katika
barabara ya Uru eneo la makelele na kuongeza kuwa Jeshi lake linamsaka mtu huyo
kutokana na kutoroka baada ya kusababisha kifo cha mwenda kwa miguu ambaye
alikufa papohapo.
No comments:
Post a Comment