MNAMO TAREHE 08.02.2013 MAJIRA YA SAA
06:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI KATA YA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL
S/O MWASALEMBA,MIAKA 18,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA ITIJI ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA
KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA PETER
S/O BOSCO,MIAKA 25,MFIPA,MPIGA DEBE,MKAZI WA ITIJI. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UCHI KANDO YA BARABARA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA KUMGOMBEA MWANAMKE ELIZABETH D/O MICHAEL, MIAKA 18,KYUSA,MUUZA POMBE ZA KIENYEJI KATIKA KILABU KIITWACHO MUSOMA MKAZI WA ITIJI. KABLA YA TUKIO MAREHEMU NA MTUHUMIWA AMBAO WOTE WALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA ELIZABETH D/O MICHAEL WALIPIGANA KILABUNI HAPO TAREHE 07.02.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS WAKIMGOMBEA MWANAMKE HUYO KISHA KUAMULIWA NA WATEJA WENGINE NA MTUHUMIWA ALIONDOKA NA MWANAMKE HUYO HADI NYUMBANI KWA MWANAMKE NA KUANZA KUMPIGA.

HATA HIVYO ELIZABETH D/O
MICHAEL ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA KURUDI KILABUNI AMBAPO ALIKUTANA NA
MAREHEMU NA KUMWELEZA TUKIO HILO AMBAYE WALIKUBALIANA KURUDI WOTE
NYUMBANI KWA MWANAMKE HUYO. MAJIRA YA SAA 01:30HRS MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO
ALIRUDI NYUMBANI KWA ELIZABETH D/O MICHAEL NA KUMKUTA MWANAMKE HUYO AKIWA
NA MAREHEMU CHUMBANI HIVYO ALIWAFUNGIA MLANGO KWA NJE NA KWENDA KUTAFUTA
KISU NA ALIPORUDI ALIVUNJA MLANGO KISHA UGOMVI BAINA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA
ULIANZA UPYA NA MTUHUMIWA ALIMCHOMA MAREHEMU KISU KIFUANI UPANDE WA
KUSHOTO NA KUSABABISHA MAREHEMU KUDONDOKA CHINI HUKU DAMU NYINGI
ZIKIMTOKA NA MTUHUMIWA KUTOWEKA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI. MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO
AMEKAMATWA KWA USHIRIKIANO BAINA YA POLISI NA WANANCHI WA ENEO HILO. TARATIBU
ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI KWA KOSA LA MAUAJI. AIDHA
MWANAMKE ANAYEDAIWA KUGOMBEWA ELIZABETH D/O MICHAEL ANAENDELEA
KUHOJIWA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. AIDHA ANATOA RAI KWA
WENYE NDOA/MAHUSIANO YA KIMAPENZI KUWA WAAMINIFU KWA WENZI WAO ILI
KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA NA PINDI WANAPOKUWA NA MIGOGORO/MATATIZO
WATUMIE NJIA YA MAZUNGUMZO KUMALIZA/TATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO.
No comments:
Post a Comment