Vichwa Vya Habari
Language
Wednesday, 6 February 2013
BURUDANI: NI KWELI ADAM KUAMBIANA ANA TABIA KAMA ZA BALOTELI? SOMA BARUA HII
MICHEZO: LEO NI TAIFA STARS AU CAMEROON???
Leo
majira ya saa 10 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki macho na masikio ya
watamazaji yatakuwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam katika mechi kati ya
Wenyeji Taifa Stars na Simba wasioshindika ikiwa ni miongoni mwa mwechi za
kirafiki kimataifa hii leo.
Taifa stars inaingia Uwanja ikiwa
na matumaini ya kushinda kwa vigogo hao wa Soka Barani Afrika walioshindwa
kutinga katika michuano ya AFCON mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.
Kocha Taifa Stars Kim Poulsen
amewataka wachezaji wake kucheza kwa kujiamini, kasi na pasi kwa sana huku
akiwatumia nyota wawili Mrisho Khalifan Ngassa(Simba SC) kwa upande wa wingi ya kushoto na Mbwana
Samatta (TP Mazembe) wingi ya kulia ikiwa ni katika kuongeza kasi.
Kwa upande wao Cameroon
hawatakuwa na nyota Samuel Eto’o anayechezea klabu ya Anzhi nchini Russia na
Alexandre Song kiungo wa zamani wa Arsenal ambayo kwa sasa anaumwa.
Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa
mwaka jana Taifa Stars iliwazaba vijana wa Rais Michael Sata, Wana Chipolopolo
bao 1-0 wakati wakiandaa na Michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini
ambao wametolewa katika hatua ya makundi.
HABARI MUHIMU: CIA ILISAIDIWA NA NCHI 54 KIUJASUSI
Shirika
la haki za binadamu la Open Society Justice Initiative, limesema mataifa 54
yalisaidia programu za shirika la ujasusi la Marekani CIA, ambapo watuhumiwa wa
ugaidi walifungwa katika magereza ya siri nje ya Marekani, au kukabidhiwa kwa
mataifa ya kigeni kwa ajili ya kuhojiwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)