Language

Wednesday, 6 February 2013

HABARI MUHIMU: CIA ILISAIDIWA NA NCHI 54 KIUJASUSI

Shirika la haki za binadamu la Open Society Justice Initiative, limesema mataifa 54 yalisaidia programu za shirika la ujasusi la Marekani CIA, ambapo watuhumiwa wa ugaidi walifungwa katika magereza ya siri nje ya Marekani, au kukabidhiwa kwa mataifa ya kigeni kwa ajili ya kuhojiwa. 
Shirika hilo limesema lilichunguza matukio ya ukiukaji wa haki za binaadamu uliohusishwa na magereza ya siri ya CIA, na operesheni za uhamishaji wa wafungwa baada ya shambulio la Septemba 11, 2001 mjini New York na Washington. Ripoti ya shirika hilo iliyopewa jina la "Globalizing Torture" inabainisha kesi za watu 136 na msaada uliyotolewa na mataifa 54. Miongoni mwa mataifa yaliyotuhumiwa kuisaidia CIA ni pamoja na washirika wa karibu wa Marekani yakiwemo Australia, Canada, Ujerumani, Uingereza na Ireland, na mengine ambayo yanatizamwa kama siyo marafiki wa Marekani kama vile Iran.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...