WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wame muua kinyama mke wa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki M. Meera Sanjeev Kumar kwa kumfunga plasta
mdomoni wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu nyumbani kwa ofisa
huyo.
Taarifa za mauaji hayo zilitolewa polisi na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa alifika Kituo Kikuu cha Polisi Oysterbay kutoa taarifa za mauaji hayo.
Akizungumza jana Kama nda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Charles Kenyela
alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambayo aliyaita ni ya kinyama na kueleza kuwa maja mbazi hao watashughulikiwa ipasavyo.
“Ni kweli kuna mauaji hayo yametokea eneo la Masaki ambako mama mmoja Meera Sanjeev Kumar (52) ameuawa majira ya saa tano usiku juzi akiwa nyumbani kwake,” alisema Kamanda Kenyela.

Alisema watu hao wanaodhaniwa ni majambazi
walifika katika nyumba hiyo iliyoko kiwanja namba 1500 na ku mfunga
kamba mikononi na miguuni na halafu plasta mdomoni na puani na
kusababisha kifo chake.
“Wakati wa tukio, mume wake aitwaye Sanjeev Kumar(56) hakuwepo nyumbani na aliporudi alimkuta mkewe akiwa kwenye kochi na tayari amekwishafariki,” alisema Kamanda Kenyela na kuongeza;
“Wakati wa tukio, mume wake aitwaye Sanjeev Kumar(56) hakuwepo nyumbani na aliporudi alimkuta mkewe akiwa kwenye kochi na tayari amekwishafariki,” alisema Kamanda Kenyela na kuongeza;
“Baada ya kukuta hali hiyo, alipatwa na mshtuko na kupiga simu polisi ambao walifika katika nyumba hiyo na kukuta mauaji hayo.”
Alisema baada ya polisi kufika walielezwa kuwa
nyumba hiyo ina walinzi watatu, lakini walikutwa wawili wakiwa wamelala
huku mmoja wao akiwa hayupo eneo hilo.
“Tulifuatilia na kubaini kuwa wale walinzi
walikuwa wako hoi baada ya kula chakula kilichokuwa kimewekwa dawa ya
kulevya ambayo yalisababisha walewe na kushindwa kujitambua,” alisema
Kamanda Kenyela na kuongeza;
“Mlinzi mwenzao wa tatu ambaye inadaiwa ndiye
aliyewapelekea chakula hicho na kuhusika na njama za kufanyika kwa
uhalifu huo alitokomea na majambazi hayo na hajulikani aliko hadi sasa.”
Kamanda Kenyela alisema hadi sasa haijulikani
kama kuna kitu kilichoibwa kwa kuwa mume wa marehemu huyo bado hajatulia
kuweza kueleza kama kuna fedha au kitu chochote kilichoibwa.
Alisema walinzi waliokuwa wanalinda nyumba
hiyo wote ni wa Kampuni ya Securex na kitendo kilichofanywa na mmoja wao
ni kusaliti lindo lao na kujihusisha na ujambazi jambo ambalo ni
hatari.
“Tunamsaka mlinzi huyo kwani amesababisha
mauaji na kwamba tabia ya walinzi kujihusisha na uhalifu inatisha kwa
kuwa kama wenyewe wanajihusisha na ujambazi basi ni hatari,” alionya
Kenyela.
Alisema ni muhimu kampuni za ulinzi zikawa
makini na watu zinaowaajiri kwa kuweka takwimu zao vizuri ili
wanapofanya uhalifu kama huo wajulikane mapema.
Kamanda Kenyela alisema hivi sasa Kinondoni kuna tishio la baadhi ya walinzi kujihusisha na ujambazi kitu ambacho kinafanya kazi ya polisi kuwa ngumu.
Alisema tishio jingine ni la madereva wa bodaboda ambao nao wamekuwa wakijihusisha kwenye ujambazi.

No comments:
Post a Comment