Jonathan Blake |
Katika taarifa ambayo GK imefuatilia kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na kupitia maoni ya wakazi wa jiji la London, imeonekana kuwa wananchi wako katika pande mbili, baadhi wakionyesha kukerwa na hatua hiyo, wakati wengioneo wakionekana kutokuwa na shida kabisa.
Kwa ufupi ni kwamba kupitishwa kwake kutapelekea kurahisisha pia kwa watu wa jinsia mmoja kuasili watoto na kuwalea kama wazazi wa asili, jambo ambalo linatatajwa kuja kuwaathiri watoto hao baadae.
Vuta picha ya ulipokuwa mtoto na ukijiandaa kwenda shule kisha unawaaga wazazi wako, kwa hawa watoto wataitaje Mama na Baba?
katika hali ya kushangaza zaidi, katika mahojianoa ambayo yamemalizika
hivi punde kupitia kituo cha shirika la utangazaji cha Uingereza, Askofu
wa Greater London, Jonathan Clive Blake ameonekana kuunga mkono na
kufurahia jambo hilo kupitishwa, akisema kwamba kila mtu ana haki ya
kuoa na kuolewa, na kuwataka watu kutowabagua wananchi wenzao.
Askofu Jonathan Blake
Kwa upande wake, muwakilishi wa muungano wa ndoa nchini humo,
"Coallition for Marriages", Dr Sharon James amesema kuwa kitendo hicho
sio cha kufurahia hata kidogo, kwani ni kinyume na maadili na hata kwa
namna ambavyo utamaduni wa ndoa unatakiwa kuwa.
Waziri Mkuu, James Cameron ni mmojawapo wa wabunge waliopiga kura ya
ndio kuafikiana na muswada huo, ambao hata hivyo umeonekana kukigawa
chama chake cha Conservative kimtazamo.
Endelea kuwa na GK, na itakuhabarisha kadri ambavyo tutaendelea kupata taarifa zaidi.
No comments:
Post a Comment