Language

Tuesday, 5 February 2013

HABARI: HII NDIO MBINU MPYA YA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA

WAKATI nchini Zimbabwe wanawake wakitumia pampers kukuza ukubwa wa makalio yao, nchini Marekani wamekuwa wakitengeneza pampers za cocaine, ambazo huvaliwa  na kusafirisha dawa hizo nchi mbalimbali pasipo kugundulika.
Mbinu hiyo mpya imedaiwa kuwagharimu muda mrefu waandaaji kutengeneza pampers hizo na baada ya kukamilika huvaliwa kitaalamu nje ya nguo zao za ndani na huvalia suruali au baibui tayari kwa kuanza safari.
Maofisa wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa JFK wamegundua mbinu hiyo mpya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwatia mbaroni wanawake wawili kutoka Bronx wakiwa wamevalia
madawa hayo. Wanawake hao wamekamatwa na kilogramu 6.5 za dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo walikuwa wamezivalia kwa mtindo wa nepi nje ya nguo zao za ndani.
Kwa mujibu wa Gazeti la Dailymail la Uingereza, wanawake hao waliokamatwa baada ya kushuka katika ndege ya  JetBlue iliyotoka Jamhuri ya Dominika huko Santo Domingo ni Priscilla Pena na Michelle Blassingale, walikamatwa wakiwa na cocaine hizo zikiwa katika mwonekano wake wa asili.
Kukamatwa kwa pea hiyo ya wanawake, kulitokana na walinzi kushangazwa na hali ya mbwa waliokuwa nao kuwafuatilia zaidi wanawake hao na kuanza kufoka ilhali walikuwa hawana mizigo, jambo lililowasukuma maofisa hao kuamua kuwakagua vilivyo.
Baada ya kuchunguza kwa makini katika mizigo yao, hawakuweza kuona madawa yoyote, lakini walipojaribu kuwavua nguo zao walikutana na idadi kubwa ya dawa za cocaine yaliyokuwa yamefungwa mithili ya pampers nyuma ya makalio yao. Baada ya kugundulika na madawa hayo haramu, wanawake hao walikamatwa na kupelekwa chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa Dailymail, Blassingale amewekwa rumande huku akisubiri kufikishwa mahakamani na Pena ameachiliwa kwa dhamana ya Dola 150,000 (sawa na Sh240 milioni). Mwezi Oktoba mwaka jana, jasusi wa dawa za kulevya alihukumiwa kifungo cha miaka 300 jela baada ya kugeuza ndege ya American Airlines kuwa chombo kikubwa cha kusafirishia dawa hizo.
Victor Baurne (37) aliyekuwa meneja mizigo wa ndege hiyo alikamatwa katika kituo hicho hicho cha (JFK) John F. Kennedy International Airport kwa kosa la kusafirisha dawa za thamani  zaidi ya Pauni 330 za cocaine toka mwaka 2000 mpaka mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...