Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF, limeelezea hofu
ya kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaouawa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
UNICEF linasema kuwa watoto hao wanajipata katika maeneo ya vita wakati
makundi yaliyojihami yanapopambana viwanjani na hata makanisani.
Aidha shirika hilo limesema kuwa takriban watoto watatu waliuawa na
wengine zaidi ya ishirini kujeruhiwa vibaya siku ya ijumaa.
Linadai kuwa watoto hao wamesajiliwa kama wapiganaji katika makundi ya
waasi.
Kumekuwa na mapigano pamoja na uporaji katika mji mkuu Bangui baada ya
waasi kuuteka mji mkuu mwezi jana.