Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF, limeelezea hofu
ya kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaouawa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
UNICEF linasema kuwa watoto hao wanajipata katika maeneo ya vita wakati
makundi yaliyojihami yanapopambana viwanjani na hata makanisani.
Aidha shirika hilo limesema kuwa takriban watoto watatu waliuawa na
wengine zaidi ya ishirini kujeruhiwa vibaya siku ya ijumaa.
Linadai kuwa watoto hao wamesajiliwa kama wapiganaji katika makundi ya
waasi.
Kumekuwa na mapigano pamoja na uporaji katika mji mkuu Bangui baada ya
waasi kuuteka mji mkuu mwezi jana.
Wiki tatu baada ya waasi wa Seleka kutwaa mamlaka katika mapinduzi ya
kijeshi,uporaji na ghasia zimekithiri nchini humo watoto wakiwa katika hatari
kubwa zaidi.
Tangu makabiliano kuanza upya mwishoni mwa mwezi wa Machi, watoto
wengine wengi zaidi wamekuwa waathiriwa wa risasi wakati wengine wakisajiliwa
kama wapiganaji. Pia kumekuwa na taarifa za kuongezeka kwa visa vya ubakaji
“Tunaiona nchi hii ikikumbwa na ghasia huku watoto wakiwa waathiriwa
wakubwa,'' alisema Souleymane Diabate afisaa mkuu wa shirika hilo katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati. ''Ghasia dhidi ya watoto lazima zisitishwe. Watu
wasio na hatia wanauawa au kujeruhiwa na lazima zichunguzwe na maafisa wakuu,''
alisema Biabate
Wiki jana UNICEF ilitoa vifaa muhimu vya matibabu na hata kuweka
kliniki ya muda kwa akina mama wajawazito ndani na nje ya mji wa Bangui. Watoto
waliojeruhiwa pia wamepokea matibabu.
No comments:
Post a Comment