Watu wengi zaidi wamejiandikisha kushiriki kwenye
marathon ya Madrid, Uspania, ya Jumapili ya mwisho wa Aprili baada ya shambulio
la bomu kwenye marathon ya Boston siku ya Jumatatu.
Waandalizi wa mbio hizo wanasema watu
waliojiandikisha ilizidi mara nne baada ya shambulio la Boston.
Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Uspania
ambayo inajitayarisha kuomba kuandaa Olimpiki ya mwaka wa 2020, alisema
wanaoshiriki kwenye marathon wakiongezeka ndio sifa kubwa ambayo watu wa Madrid
wanaweza kuupa mji wa Boston.
No comments:
Post a Comment