Bunge la uteuzi nchini China limemteua kiongozi wa Chama cha Kikomunisti,
Xi Jinping, kuwa rais hatua inayomuweka kwenye kilele cha madaraka ya taifa
hilo linalokuwa kwa kasi kubwa ya kiuchumi duniani.
Xi Jinping aliinama kwa heshima juu ya jukwaa kuu katika Ukumbi Mkuu wa
Watu wa China, kama linavyoitwa jengo la bunge la nchi hiyo, huku wajumbe
wakimpigia makofi ya kumpongeza katika tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na
televisheni ya taifa.