Vyombo vya sheria nchini Nigeria vimemsamehe gavana wa zamani Diepreye
Alamieyeseigha aliyeshutumiwa kuiba mamilioni ya dola kutoka kwa serikali.
Msamaha huo ulitolewa na baraza la serikali, linalojumuisha rais Goodluck
Jonathan ambaye aliwahi kuhudumu chini ya bwana Diepreye.
Mwandishi wa BBC nchini humo amesema kuwa hatua hiyo, ambayo imepingwa
vikali na wanaharakati dhidi ya ufisadi, inamaana kuwa bwana Diepreye
ataruhusiwa kuwania wadhifa wa kisiasa.
Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Bayelsa ambaye alitiwa nguvuni nchini
Uingereza mwaka wa 2005 alikwepa kifungo kwa kukimbilia nchini Nigeria akiwa
amevaa mavazi ya kike.
Amehudumu siku mbili tu ya kifungo cha miaka miwili aliyohukumiwa.
No comments:
Post a Comment