Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya asili mia 28% ya
wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi, ikilinganishwa na asili mia
4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka kwa mababa sukari au
kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na wasichana wadogo kwa umri).
Waziri Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana
wengi wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa
na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asili mia kumi ya raia wa
Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo imekuwa na mradi wa kuvuma
zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais
Jacob Zuma alipomteua bwana Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata
miaka minee iliyopita.
'Kupotosha watoto'
Waziri huyo pia aliongeza kuwa zaidi ya wasichana 94,000 walipata mimba
katika mwaka wa 2001 and kati yao 77, 000 walilazimika kuavya mimba hizo katika
kliniki za serikali, kwa mujibu wa taarfa katika magazeti ya Soweto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Carolina, mkoa wa
Mpumalanga, bwana Motsoaledi alisema kuwa idadi hiyo kubwa ya wasichana wanaoharibiwa
maisha yao ''inanivunja moyo sana''.
''Lazima tuchukue hatua dhidi ya mababa sukari hawa kwasababu
wanaangamiza vizazi vyetu''.
Mwaka uliopita zaidi ya watu 260,000 wanaoishi na Ukimwi walifariki
ikiwa ni takriban nusu ya watu wote waliofariki katika nchi hiyo
No comments:
Post a Comment