Language

Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

Friday, 3 May 2013

KAMA NA WEWE UNASUMBULIWA TATIZO LA KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO LA NDOA, PATA SULUHISHO HAPA


Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya Robo (25%) ya wanaume duniani kote husumbuliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa na kushindwa kurudia tena mchezo!

Sababu ya tatizo hili huweza kuwa ya Kibaiolojia na Kiakili. Kama wewe pia ni moja yao na unapenda kujua jinsi ya zuia hali hii, endelea kusoma.

• Jenga tabia ya kufanya mazoezi:
Mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwahiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujenga tabia ya kufanya mazoezi ambayo husaidia kukujengea afya njema na kukupa mzunguko mzuri wa damu. Kama una mwili wenye afya basi inaweza kukusaidia kwa namna ya kifikra ambazo huchangia kwenye swala zima la kuwahi kupizi. Hii hutokana na hutokana na kuongeza kujiamini na kujihusudu.
 • Pumua vizuri na kikamilifu:
Kiungo chochote cha mwili huhitaji nguvu kamili ili kufanya kazi na ndivyo ilivyo kwa habari ya viungo vya uzazi! Unapo pumua vizuri na kwa ukamilifu, kiungo hiki hupata nguvu za ziada. Mbinu mbalimbali za kupumua kama pranayama hujajwa kusaidia sana kujifunza jinsi ya kuzuia kupizi mapema. Baada ya kuinza tu (wakati wa tendo), jaribu kupumua kwa ufasaha ili mwili uweze kupata hisia kabla ya kuanza kufanya msuguano.
 • Mshirikishe mwenzako kikamilifu:
Kuridhika kimapenzi ni tukio ambalo wote wawili mnaridhika kikamilifu. Ili kujifunza kujizuia kukojoa haraka, ni vizuri kuwasiliana na mwenzi wako wa kimapenzi. Anaweza akakusaidia kushinda tatizo hili la kiaibu, kila unapohisi unataka kukojoa mapema, sema 'ngoja' na usitishe kwanza shughuli zote kwa muda kidogo.

Thursday, 2 May 2013

VIWANDA VINNE VIMEFUNGWA KILIMANJARO


VIWANDA vinne vya kutengeneza pombe, kusindika maziwa na machinjio mawili yamefungwa katika wilaya za Rombo, Mwanga na Siha mkoani Kilimanjaro kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya ubora vilivyoainishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

 Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kaskazini, Abdalah Mkanza alisema ufungaji huo umefanikiwa wakati idara ya ukaguzi ya kanda hiyo ilipofanya ukaguzi wa kushitukiza kwa kushirikiana na wakaguzi wengine kutoka Kanda ya Mashariki.
Alisema ukaguzi ulifanyika kwa viwanda vyote vikubwa na vidogo mkoani Kilimanjaro na machinjio yote za mjini na vijijini ambapo walibaini wananchi wapo hatarini kupata magonjwa kutokana na mazingira halisi ya uchinjajio wa wanyama na viwanda hivyo.
Mkaguzi huyo alisema zoezi la ukaguzi litafanyika kwa mara nyingine mkoani humo kwa lengo la kutazama iwapo maeneo waliyoyapa maelekezo yamefuata ama la, ili hatua nyingine ziweze kuchukuliwa iwapo itabainika wamepuuza.
Aliwataka wafanyabiashara na waagizaji wengine wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuwasiliana na TFDA ili kujiridhisha kama wanavyoagiza au kutumia kwa ajili ya walaji vimethibitishwa na mamlaka hiyo.

ZISOME HAPA FAIDA KUBWA ZA KUFANYA MAPENZI


Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kuongeza mwendo wa damu Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.
 Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, piahuondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Tuesday, 16 April 2013

MUHIMBILI KWISHA HABARI YAKE, NI WAGONJWA 7 TU WANAOWEZA KUHUDUMIWA



Kituo cha Afya ya Akili cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kilichopo Chamazi Mbagala kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa saba tu imefahamika.

Hali hiyo imekuwa ikisababisha wagojwa wengi wenye tatizo hilo kushindwa kupata huduma au kupata katika hali isiyo na ubora.
Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Agrey Mwanri, alisema awali kituo hicho kilikuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 32.
Mwanari alisema kutokana na kituo hicho kuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa wachache, Hospitali ya Muhimbili haipeleki wagonjwa katika kituo hicho kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Mwanri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi (CCM), aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuendeleza kituo hicho ambacho ni muhimu kwa wagonjwa wa akili.

Monday, 18 March 2013

AFYA: AFYA YA MAMA NA MTOTO

Ikiwa mama na mtoto wanaishi na VVU na wanatumia dawa, watumie dawa kama walivyoshauriwa na mtoa huduma wa afya. Dawa zote zihifadhiwe vizuri.

AFYA: TUMIA VEMA VYOMBO VYA MAWASILIANO KULINDA AFYA YAKO


WATANZANIA wametakiwa kuwa na matumizi sahihi ya Kompyuta, Televisheni na Simu ili kuepusha athari katika miili yao.

Akizungumza katika Kanisa la Tanzania Assembiles of God Amani Cathedral Centre kwa Mchungaji Benjamin Bukuku, Mwezeshaji Konya Alex amesema vifaa hivyo ni muhimu katika utendaji wa kazi hususani katika Ulimwengu huu wa digitali.
Konya amesema watanzania hawatakiwi kuviacha kuvitumia kutokana na ukweli kwamba vina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku hivyo umakini katika kutumia utapunguza athari katika miili ya binadamu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...