WATANZANIA wametakiwa kuwa na matumizi sahihi ya Kompyuta, Televisheni na
Simu ili kuepusha athari katika miili yao.
Akizungumza katika Kanisa la Tanzania Assembiles of God Amani Cathedral
Centre kwa Mchungaji Benjamin Bukuku, Mwezeshaji Konya Alex amesema vifaa hivyo
ni muhimu katika utendaji wa kazi hususani katika Ulimwengu huu wa digitali.
Konya amesema watanzania hawatakiwi kuviacha kuvitumia kutokana na
ukweli kwamba vina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku hivyo umakini
katika kutumia utapunguza athari katika miili ya binadamu.
No comments:
Post a Comment