Mahakama kuu ya mjini Mogadishu Somalia imemwaachilia huru mwandishi
wa habari ambaye alifungwa kwa sababu ya kumhoji mwanamke aliyesema amebakwa.
Katika kesi iliyolalamikiwa kimataifa, mwandishi huyo, Abdilaziz
Abdinuur, awali alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja kwa kumhoji mwanamke
ambaye alisema alibakwa na wanajeshi wa serikali.
Mwanamke huyo piya alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja lakini kesi yake
ilifutwa kwenye rufaa awali mwezi huu.
Jaji wa mahakama makuu - Aidid Abdulahi Ilkahanaf - alisema mashtaka
yote dhidi ya mwandishi huyo wa habari sasa yamefutwa.
No comments:
Post a Comment