Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba,
unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta
mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha
mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.
Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo
ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kuongeza mwendo wa damu Tendo la ndoa
husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya
viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha
mfumo wa upumuaji.
Msukumo thabiti wa damu mpya
yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya
damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, piahuondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha
mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol)
nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta
yenye kileo mwilini.
Kupunguza maumivu.
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini
ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza
maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo
(Whiplash) na maumivu ya kichwa.
Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)
Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi
husababisha kuleta matatizo mwilini.
Tendo la ndoala mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye
madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo
yahusianayo na tezi ya prostate. Kupunguza mfadhaiko wa moyo.
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza
akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la
ndoa wanatajwa kushinda
mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike
likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka
zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.
Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za
kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.Kuishi muda mrefu huku
ukionekana kijanaWakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA uzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko
wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu
duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu,
kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo
(Cardiovascular).
Hupunguza baridi na mafua. Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la
ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe
hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili
dhidi ya magonjwa.
Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
NB : Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa
ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa.
No comments:
Post a Comment