Watu kadhaa akiwemo mbunge wa upinzani wamekamatwa katika mji mkuu wa
Chad Ndjamena, katika kile ambacho serikali inasema ilikuwa njama ya kuvuruga
hali nchini humo.
Taarifa kutoka kwa vyombo vya serikali zinasema kuwa kundi moja dogo la
watu limekuwa likipanga njama hiyo kwa miezi minne.
]Viongozi wa njama hiyo ya mapinduzi wanachunguzwa na wendesha
mashtaka.
Chad ina historia ndefu ya mapinduzi na uasi. Rais wa sasa Idriss Deby
mwenyewe alichukua mamlaka kwa njia ya mapinduzi mwaka 1990.
Serikali ilisema kuwa kundi moja la watu wenye nia mbaya walijaribu
kufanya mapinduzi dhidi ya taasisi za nchi.
Ilisema kuwa maafisa wa usalama wa serikali walikabiliana nao bila
kutaja idadi yao.
Polisi pamoja na duru za upinzani zilisema kuwa mbunge huyo Saleh Makki
alikuwa miongoni mwa waliokamatwa.
Pamoja na waliokamatwa ni wanajeshi kadhaa
Tangu nchi hiyo kujipatia uhuru kutoka kwa Ufaransa, mwaka 1960, Chad
imekumbwa na misukosuko hasa kati ya eneo la Kaskazini ambalo lina waarabu
wengi na Kusini ambako kuna wakristo wengi.
Mapema mwaka huu Chad iliwapeleka wanajeshi 2,000 kujaribu, kuwatimua
wapiganaji walioteka sehemu kubwa ya Mali.
No comments:
Post a Comment