Katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne, rais Obama alisema
nchi yake haiweze kuendelea kuwaweka watu hao katika eneo lisilo katika himaya
ya nchi yoyote milele.
Obama alibainisha hoja zake za
kulifunga gereza hilo, akisema kuwa uendeshwaji wake umekuwa na gharama kubwa
huku likikosa ufanisi, na kwamba linaathiri sifa ya Marekani katika jamii ya
kimataifa, na kupunguza ushirikiano na washirika wake katika vita dhidi ya
ugaidi.
Obama alisisitiza kuwa ni muhimu kuelewa kuwa Guantanamo siyo muhimu
kuifanya Amerika kuendelea kuwa salama. "Wazo kwamba tutaendelea kuliweka
kundi la watu ambao hawajashtakiwa kwa muda mrefu, ni kinyume na utamaduni wetu
na laazima jambo hilo likome," alisema.
No comments:
Post a Comment