Kufuatia hali hiyo waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, ametishia kuwa
serikali yake itafanya kila liwezekanalo hata kama ni kutumia jeshi ili kulinda
usalama wa raia wa Korea Kusini waliokuwa wakifanya kazi katika eneo hilo
ambalo linatumiwa na Korea mbili.
Meneja wa moja ya viwanda katika eneo hilo, Lee Jae-Young, akiongea na
Shirika la habari la AFP amesema, hatua hiyo imeathiri mzunguko wa biashara na
uzalishaji baada ya malighafi nyingi za viwanda hivyo zinazosafirishwa kwa meli
kwenda eneo la Kaesong kwa ajili ya uzalishaji, kukwama.
No comments:
Post a Comment