Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano wa Wanaume
Halisi na Wanaume Family wamemtunuku Juma Kassim ‘Nature’ kuwa Mfalme wa Temeke
kutokana na jinsi walivyomkubali na kumwamini.
Mpambano huo ulioteka hisia za watu wengi, ulipigwa Jumapili iliyopita
katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, jijini Dar ambapo mbali na umati
mkubwa wa mashabiki hao kumshangilia Juma Nature na kundi lake, walionyesha
kukubali onyesho la Wanaume Family walipokuwa jukwaani.
Umati wa mashabiki ulipiga mayowe ya furaha kuonyesha kuwa wamekubali
zaidi onyesho la Wanaume Family kuliko hata lile la Wanaume Halisi haswa
walipokuwa wakitumbuiza nyimbo zao zinazopendwaukiwemo Dar Mpaka Moro, Mkono
Mmoja, pamoja na nyingine nyingi kali ambazo walinogesha zaidi walipokuwa
wakirusha miguu hewani kwa mtindo wa ‘mapanga shaa’.
Baada ya kila kundi kupanda jukwaani kwa awamu mbili tofauti, jaji wa
mpambano huo John Dilinga ‘DJ JD’ aliwataka mashabiki kumtaja Mfalme wa Temeke
ambapo walijibu kwa pamoja; “Nature” hivyo kumfanya mkali huyo
anayewakilisha kundi la Wanaume Halisi kuwa Mfalme wa Temeke ingawa kwa
namna moja au nyingine walikubali zaidi onyesho la Wanaume Family, lakini
mapenzi yao yako kwa kinara huyo.
Mbali ya onesho kali la mpambano huo, mkongwe kwenye muziki wa Hip Hop
nchini, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na
Inspector Haroun waliutumia vyema muda wa mapumziko ya mpambano huo kutumbuiza
nyimbo zao zinazobamba.
No comments:
Post a Comment