Mrembo Salha Israel, ambaye alivaa taji la Miss Tanzania mwaka 2011/2012
ameamua rasmi kuingia kwenye tasnia ya uigizaji baada ya msimu wake wa urembo
kuisha.

Salha ameiambia Mwananchi kwamba amechagua uigizaji kuwa kazi yake mpya
kwa sasa, na kwamba mashabiki wategemee mengi kutoka kwake
Akiongeza kwenye mazungumzo hayo Miss Tanzania huyo ambaye alimaliza
kutumikia taji lake vizuri bila kupata skendo zozote mbaya alisema,”Kufanya
movie ilikuwa ni moja ya ndoto zangu kubwa. Nilikuwa na mawazo kwamba hata
ningeshindwa kupata taji la Miss Tanzania basi ningeingia moja kwa moja kwenye
uigizaji. Lakini ilinibidi nisubili kidogo baada ya kushinda taji lile na muda
ndio huu umefika”.
Salha hatakuwa mrembo wa kwanza kuingia kwenye uigizaji kwani Wema
Sepetu, Aunty Ezekiel na Irene Uwoya ambao wote ni baadhi ya waigizaji wa kike
wanaofanya vizuri hivi sasa kwenye uigizaji, wamepata umaarufu kwanza kupitia
mashindano ya urembo Tanzania maarufu kama Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment