Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela anaendelea kupata nafuu
wakati akitibiwa homa ya mapafu, kwa mujibu wa madaktari wake.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, ilisema kuwa Mandela
alitembelewa na jamaa zake wakati akiendelea kupokea matibabu.

Mandela amelazwa hospitalini sasa kwa mara ya nne katika kipindi cha
miaka miwili.
Mnamo Disemba alitibiwa homa ya mapafu na kibofu na alikaa hospitalini
sana kuliko wakatii mwingine wowote.
Mnamo Februari alitibiwa maradhi ya tumbo.
Wiki jana rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94,pia alibitiwa
maradhi ya mapafu.
Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu muda atakaosalia kuwa
hospitalini.
Bwana Mandela alikuwa rais wa Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi 1999
na anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa hilo kwa kupigana dhidi ya enzi ya
utawala wa ubaguzi wa rangi.
Licha ya kufungwa kwa miaka mingi jela, Mandela alisema aliwasamehe
maadui zake na kuwataka wananchi wa taifa hilo kushirikiana.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993
No comments:
Post a Comment