Language

Saturday, 9 February 2013

MICHEZO: MESSI ASAINI MKATABA MPYA BARCA MPAKA 2018

MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amesaini mkataba mpya na Barcelona, ambao utamfanya aichezee klabu hiyo hadi Juni 30 mwaka 2018, vinara hao wa Ligi Kuu ya Hispania.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amesaini mkataba ambao alifikia makubaliano Desemba, mwaka jana ambao unahusisha pia miaka miwili aliyobakiza katika mkataba wake wa sasa na atapiga kazi Nou Camp hadi akiwa na miaka 31.

Nahodha huyo wa Argentina, alijiunga na timu ya vijana ya Akademi ya Barcelona, akiwa ana umri wa miaka 13 na alianza kuchezea timu ya wakubwa, akiwa ana umri wa miaka 16.

Messi ni mfungaji bora wa kihistoria wa Barca, amekuwa mfungaji bora kwenye Ligi ya Mabingwa kwa miaka minne iliyopita na ameweka rekodi ya kumaliza kalenda ya mwaka na mabao 91 kwa klabu na nchi yake mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...