MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Ivory Coast, Didier Drogba amepata mapokezi mazuri alipowasili Istanbul
alipokubali kujiunga na Galatasaray ya Uturuki katika uhamisho wa Januari.
Kiungo wa
zamani wa Inter Milan, Wesley Sneijder alipata mapokezi kama hayo alipowasili
Uturuki mwezi uliopita na Drogba ameamua kumfuata Mholanzi huyo akiondoka
Shanghai Shenhua ya China.
Nahodha
huyo wa Ivory Coast alichelewa kuwasili kwenye timu hiyo kwa sababu ya Fainali
za Mataifa ya Afrika.
Drogba
ataungana na Emmanuel Eboue, ambaye alijiunga na klabu hiyo bingwa ya Uturuki
akitokea Arsenal mwaka 2011.
Mshambuliaji
mwingine wa zamani wa Chelsea, ambaye alitoka Stamford Bridge kwenda China,
Nicolas Anelka amerejea Ulaya.
Nicolas
Anelka alijiunga na Shenhua Januari mwaka jana, lakini ameamua kujiunga na
vigogo wa Italia, Juventus, akikamilisha uhamisho wake kwa mabingwa hao wa
Serie A mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment