Language

Thursday, 24 January 2013

MITINDO: FLAVIANA MTATA ASHINDA TUZO YA MWANAMITINDO BORA MWENYE MVUTO ZAIDI AFRIKA

FLAVIANA Matata, mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania, ameshinda tuzo ya ‘Nigeria’s Next Super model 2012’ inayomtambulisha kama Mwanamitindo Bora mwenye Mvuto Afrika (Africa’s Most Outstanding Model 2012).

Ushindi wa tuzo hiyo ya pekee kwa aina yake, umefungua milango ya kutambulika zaidi Matata hata kulivusha kimataifa jina la Tanzania katika tasnia ya mitindo na mavazi.
Akiongelea ushindi wa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema ushindi wa Matata ni mafanikio mengine ya kujivunia. Tsehai ndiye aliyevumbua kipaji cha Matata.
Kwa mara ya kwanza Flaviana aliibuka kwenye mashindano ya Miss Universe akiweka rekodi ya mrembo wa kwanza kushinda taji hilo nchini.
Aliiwakilisha nchi kwenye mashindano ya ‘World Miss Universe’ mwaka 2007 na kumaliza nafasi ya sita, mjini Mexico City, Mexico.
Matata pia ni balozi wa taasisi ya kusaidia watoto (SOS) na Matata Diamond Empowerment Fund (Def) ya Marekani, ambapo anafanya kazi sambamba na mwanamitindo na msanii wa vipindi vya televisheni Kim Kardashian.
Kimwana huyo pia ana mkataba na kampuni ya mitindo ya Afrika Kusini inayojulikana kama Boss Models SA, ambapo awali pia aliwahi kufanya kazi na
Kampuni ya Models pia ya Afrika Kusini.
Kwa sasa makazi yake yako mjini New York, Marekani ambapo pia anafanya kazi za mitindo katika Miji ya London, Paris na Milan.
Tuzo hiyo imeboresha zaidi fursa yake kutambulika kimataifa tangu alipoibuka mara ya kwanza nchini kupitia mashindano ya urembo.
Miongoni mwa mafanikio aliyopata kupitia sanaa ya mitindo ni umiliki wa taasisi binafsi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo amekuwa akisomesha watoto wa kike kila mwaka.
Aidha, aliwahi kushinda tuzo ya mwanamitindo bora ya jarida la kila wiki Nigeria ‘Arise Magazine Fashion’ mjini Lagos mwaka juzi.
Pia aliwahi kuingia kwenye orodha ya wanamitindo bora 10 wenye asili ya Afrika waliotangazwa na jarida la Essence Magazine.
Isitoshe, umaarufu wake ulimpa  nafasi ya kushirikiana na wanamitindo mbalimbali wa kimataifa na miongoni mwao ni Tommy Hilfiger, Jason Wu, Alexander McQueen na SUNO.
Wengine katika orodha hiyo ni Catherine Malandrino, Ally Rehmtullah, Rachel Roy, Charlotte Ronson, Tony Burch na Vivienne Westwood.
Majarida mbalimbali ya kimataifa yametumia picha zake kadhaa na hii ni kwa sababu ya mafanikio yake kwenye sanaa ya mitind

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...