Baraza la Senate nchini Brazil, limepitisha bila pingamizi, mswaada wa
kihistoria unaowapa haki sawa wafanyakazi wa majumbani na wale na maofisini
kote nchini.
Sheria hiyo mpya, inafafanua idadi ya siku za kazi ambazo wafanyakazi
hao pamoja na wapishi wanaweza kufanya kazi na hata kiwango cha ziada cha
marupuupu watakachopata.
Mageuzi hayo ya kikatiba yataanza kutekelezwa wiki ijayo wakati ambapo
rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff atatia saini,mswaada huo.
Mswaada huo unaojulikana kama mswaada wa wafanyakazi wa majumbani, una
uwezo wa kutikisa tamaduni za nchi hiyo kuhusiana na ajira ya wafanyakazi hao.
Kwa mara ya kwanza, sawa na wafanyakazi wengine wanaoajiriwa kwa
mikataba , wafanyakazi, wa majumbani nchini Brazil wataruhusiwa kufanya kazi
kwa masaa manane kwa siku na kulipwa pesa za ziada kwa masaa zaidi
watakavyofanya kazi pamoja na marupurupu mengine yanayotolewa kwa wafanyakazi
wengine nchini humo.
Wakati wa kipindi cha kupigia kura mswaada huo, maseneta waliutaja
mswaada huo kama wa kihistoria ambayo unafutilia mbali tabia ya utumwa.
Kwa kawaida familia nyingi za kipato cha kadri nchini Brazil, huwaajiri
wapishi na wafanyakazi ambao wakati mwingine wanaishi na waajiri wao.
Katika miaka ya hivi karibuni, wafanyakazi wa majumbani wamekuwa
wakipewa haki wanazostahili kama kupewa likizo na pia kupewa muda wa mapumziko
wakati wanapojifungua mimba.
Mabadiliko hayo huenda yakaongeza gharama ya kuwaajiri wafanyakazi wa
majumbani kwa asilimia ishirini.
Kulingana na shirika la wafanyakazi duniani,Brazil ndio nchi yenye
idadi kubwa ya wafanyakazi wa majumbani duniani wakiwa milioni saba.
No comments:
Post a Comment