Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya
ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne.
Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye ni waziri
mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha,
James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed
ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini
amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya
yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja
mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge
Justin Muturi.
Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu
wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.
No comments:
Post a Comment