Language

Wednesday, 6 February 2013

MICHEZO: LEO NI TAIFA STARS AU CAMEROON???

Leo majira ya saa 10 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki macho na masikio ya watamazaji yatakuwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam katika mechi kati ya Wenyeji Taifa Stars na Simba wasioshindika ikiwa ni miongoni mwa mwechi za kirafiki kimataifa hii leo.
Taifa stars inaingia Uwanja ikiwa na matumaini ya kushinda kwa vigogo hao wa Soka Barani Afrika walioshindwa kutinga katika michuano ya AFCON mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.
Kocha Taifa Stars Kim Poulsen amewataka wachezaji wake kucheza kwa kujiamini, kasi na pasi kwa sana huku akiwatumia nyota wawili Mrisho Khalifan Ngassa(Simba SC)  kwa upande wa wingi ya kushoto na Mbwana Samatta (TP Mazembe) wingi ya kulia ikiwa ni katika kuongeza kasi.
Kwa upande wao Cameroon hawatakuwa na nyota Samuel Eto’o anayechezea klabu ya Anzhi nchini Russia na Alexandre Song kiungo wa zamani wa Arsenal ambayo kwa sasa anaumwa.
Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa mwaka jana Taifa Stars iliwazaba vijana wa Rais Michael Sata, Wana Chipolopolo bao 1-0 wakati wakiandaa na Michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini ambao wametolewa katika hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...