Language

Sunday, 14 April 2013

AUNT EZEKIEL AMLILIA KANUMBA KABURINI PEKE YAKE!!!



STAA kiwango wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amenaswa kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba peke yake baada ya watu wote kuondoka.

Tukio hilo lilitokea juzikati katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo tofauti na wasanii wengine waliofika kumuenzi marehemu aliyekuwa akitimiza mwaka mmoja kaburini, Aunt alibaki peke yake, akapiga magoti kaburini na kuanza kulia kwa uchungu.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika makaburi hayo, walishangazwa na tukio la Aunt kukaa makaburini kwa takribani dakika kumi huku wengine wakimuonea huruma kutokana na msanii huyo kushindwa kuzuia hisia zake.
“Kiukweli kila nikifika katika kaburi la Kanumba lazima nihisi kuchanganyikiwa. Kuna wakati mwingine siamini kabisa kama huyu mtu hatunaye tena hivyo nahitaji kubaki hata peke yangu kaburini nimsalie kisha niondoke,” alisema Aunt huku akifuta machozi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...