Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema
kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015,
iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati
huo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya
kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius
Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika
nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa
ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati
utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri
nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa
Bunge.
Bunge.
Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa
kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi
ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... “Sina sababu za kuanza
kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa
watu sasa,” alisema Sitta.
Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa
kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema
endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi
wa kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.
No comments:
Post a Comment