KESI ya madai inayomkabili aliyekuwa Mtawa wa Shirika la
Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani
anayedaiwa kufumaniwa na mume wa mtu imepangwa kusikilizwa Januari 29
mwaka huu.
“Sista’ Yasita licha ya kuwa mtumishi wa afya
katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa lakini inadaiwa
ameachana na maisha ya kitawa miaka miwili iliyopita kwa hiyari
yake akiwa Mtawa wa Shirika la Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa
Afrika (MMMA).
Shauri hilo la madai linatarajiwa kuanza
kusikiliza katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa, mbele ya Hakimu
Jaffari Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh3
milioni baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa aitwaye Martin Msangawale
(39), Mhasibu wa Manispaa ya Sumbawanga.
Siku hiyo ya kusikilizwa kwa shauri hilo
mlalamikaji katika shauri hilo Asteria anatarajiwa kuwaleta
mashahidi wake wanne mahakamani hapo
.
.
Katika hati ya awali ya madai inadaiwa kuwa
mshtakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa
kwenye nyumba ya kulala wageni ya Chipu iliyoko eneo la Katandala mjini
Sumbawanga usiku wa Desemba 24 mwaka jana siku ya mkesha wa Sikukuu
ya Krismasi. Hakimu, Mkinga alisema kuwa kesi hiyo iliyokuwa
isikilizwe Januari 21 imeahirishwa hadi Januari 29 mwaka huu ili
kumapatia mlalamikaji muda wa kuwaleta mashahidi wake mahakamani.
Mlalamikaji wa shauri hilo la madai, Asteria
amedai nje ya mahakama kuwa alifunga ndoa ya Kikristu na mumewe
huyo Martin Msangawale mwaka 2007.
Kesi hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi hususani wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake kutokana na kuwa gumzo kubwa na kuteka hisia za watu wengi hivi sasa.
Kesi hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi hususani wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake kutokana na kuwa gumzo kubwa na kuteka hisia za watu wengi hivi sasa.
No comments:
Post a Comment