IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi
na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona
yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.
Risasi
Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na
imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo
za umeme
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema
watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za
awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu
zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo
ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa
masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu
yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni
ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo
utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye
nembo yetu,” alisema mtu huyo.
Mwandishi wetu alifika katika Hoteli ya Kindoroko iliyopo mjini hapa
juzi, Jumapili Februari 10, mwaka huu, akaonana na mtu wa mapokezi na
kujitambulisha kama mwanachama mpya anayetaka kuonana na mhusika
aliyepanga chumba namba 87.
Cha kushangaza, mhudumu alimwambia hawana
mteja wa aina hiyo katika hoteli yao na kwamba hakuna chumba chenye
namba aliyoelekezwa, jambo lililoonesha wazi kuwa wahusika ni matapeli
wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Naye meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara alipopigiwa simu, alitoa majibu kama ya mtu wa mapokezi.
Upekuzi
wa gazeti hili umebaini kuwa, simu namba 0714 084841 iliyotakiwa
kutumiwa fedha na mtu aliyejiita wa Freemasons imesajiliwa kwa jina la
Flora Tuvana.
No comments:
Post a Comment