Wakenya watakwenda kupiga kura hapo Machi 4 kumchagua kiongozi
atakayeiongoza nchi hiyo. Wagombea wa kiti cha urais watafanya mjadala
wa
pili kujieleza juu ya yale watakayoyafanya pindi wakichaguliwa.
Mjadala wa huu wa sasa utashughulikia masuala makuu ya uchumi na ardhi pamoja na mambo mengine. Kwa kutaka kufahamu zaidi Sekione Kitojo amezungumza na Mwenyekiti wa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanaojihusisha na ardhi (Kenya Land Alliance) Odenda Lumbumba ambaye kwanza alitaka kujua kwa nini hivi sasa suala la ardhi limepata kipaumbele zaidi. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.
No comments:
Post a Comment