Umoja wa Mataifa umemteua Generali mmoja raia wa Brazil ambaye anasifika
kwa kudhibiti mtaa mmoja wa mabanda nchini Haiti kutokanamana na vurugu kuweza
kuwaongoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi
20,000, ikiwemo kikosi kipya cha wanajeshi kitakachopambana na waasi mashariki
mwa nchi.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Umoja wa mataifa kukabidhi kikosi cha
wanajeshi nguvu kuweza kupambana na waasi.
Generali Santos Cruz, aliambia BBC kuwa wanajeshi wake, watafunzwa
namna watakavyo pambana na waasi bila kuwajeruhi raia na kuharibu mali nchini
Congo.
"eneo tete zaidi siku hizi ni Mashariki mwa nchi,'' Cruz alimbia
BBC
"niko tayari kukabiliana, na hali ngumu zaidi. Lengo kuu ni
kuwaondolea hali ngumu wanayokabiliana nayo watu wa Congo.''
Generali Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 2,500, wakiwa na
jukumu la kuwapokonya silaha waasi pamoja na kuwarejesha katika maisha ya
kiraia Mashariki mwa DR Congo.''
Kikosi cha walinda amani cha Umoja wa mataifa,kilichoko Congo
kimekosolewa sana kwa kukosa kumaliza vita, vya miongo miwili.
Wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini ndio walio
wengi katika kikosi hicho na wataanza kazi yao mwezi Julai.
Generali Santos Cruz ni kamanda mstaafu, wa kikosi kilichowahi kutumwa
nchini Haiti, na anasifiwa kwa kupambana vikali na megenge ya majambazi nchini
Humo mwaka 2007
No comments:
Post a Comment