Language

Friday, 11 January 2013

UN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI MALI


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alihoji ikiwa rais Dioncounda Traore alikuwa ametoa ombi maalum na kufafanua aina ya msaada anaotaka. 

Ufaransa inatarajiwa kutoa jibu lake leo wakati wa mkutano wa dharura utakaofanyika , kwa mujibu wa balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Gerard Araud.
Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mpango wa kutuma wanajeshi elfu tatu kuweza kutwaa eneo la Kaskazini mwa nchi ambalo linadhibitiwa na makundi ya kigaidi yaliyo na uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Wapiganaji wa kiisilamu wameweka sheria kali za kiisilamu katika eneo hilo.
Kwa sababu ya mipango ya usafiri na vifaa , kikosi cha wanajeshi wa Afrika hakitatarajiwa kuanza kazi hadi ifikapo Septemba au Oktoba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...