
Sulemain Abu Ghaith ambaye ni mwanamgambo aliyeonekana katika mikanda
ya video akiwakilisha mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda baada ya mashambulio
Septemba mwaka 2001,alikamatwa nchini Uturuki wiki iliyopita na kusafirishwa
hadi Marekani kushitakiwa.
Abu Ghaith aliyezaliwa Kuwait amekuwa msemaji wa mtandao huo wa kigaidi
na alikuwa mshirika wa karibu sana wa baba mkwe wake,Osama. Amekuwa akisifia
sana mashambulio ya kigaidi ya septemba 11 mwaka 2001 na kuonya kuwa kutakuwa
na mashambulio hata zaidi.
Kesi dhidi yake ni ushindi mkubwa kisheria kwa utawala wa Rais Barrack
Obama ambao umekuwa ukitafuta kwa muda mrefu kuwashtaki washukiwa wakuu
wanaohusishwa na Al Qaeda badala ya kuwazuia tu katika kambi ya kijeshi ya
Guantanamo Bay iliyoko Cuba. Kuwashtaki washukiwa wakuu wa kigaidi katika
mahakama za Marekani ilikuwa mojawapo ya ahadi kuu alizotoa Rais Obama punde tu
baada ya kuchukua madaraka mwaka 2009 akilenga kufunga kambi hiyo ya Guantanamo
Bay.
No comments:
Post a Comment