Mkuu wa jeshi la Guinea, ameuawa kwenye ajali ya ndege katika nchi jirani ya Liberia, akiwa na maafisa wegine watano.
Waliarifiwa kuwa hapakuwa na manusura wa ajali hiyo lakini haikufahamika mara moja idadi ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Baadhi walisema kuwa ni wanajeshi 18 waliokuwa wameabiri ndege hiyo.
Kwa mujibu wa waziri wa habari ,ndege yenyewe ilianguka mjini Charlesville, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Liberia.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirlief, alizuru eneo la ajali, Kusini mwa Monrovia.
Kulingana na shirika la habari la AP, kifo cha Jenerali Diallo, kilitangazwa na rais wa Guinea.
Rais alielezea kusikitishwa na habari za kifo hicho, alipokuwa anakitangaza.
No comments:
Post a Comment