Serikali ya Zimbabwe haitaruhusu wasimamizi wa nchi za Magharibi kuja
kusimia kura ya maoni ya katiba mpya wiki ijayo na uchaguzi mkuu utakaofanyika
katikati ya mwaka huu.
Serikali ya Rais Robert Mugabe imesemakuwa haitaruhusu wasimamizi
kutoka mataifa ya Magharibi kuja nchini Zimbabwe kusimia zoezi la utoaji maoni
kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo wiki ijayo. Sambamba na hayo pia iserikali hiyo
imedai hakutakuwa na haja ya kuja wasimamizi hao katika uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika katikati ya mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nje wa Zimbambwe Simbarashe Mumbengwi ameiambia DW
kuwa Umoja wa Ulaya pamoja nchi nyingine za Magharibi hawataruhusiwa kuingia
nchini Zimbabwe kwa ajili ya kusimamia utoaji wa maoni unatarajiwa kufanyika
juma lijalo na kwenye uchaguzi utakaofanyika katikati ya mwaka huu. Amesama
wasimamizi kutoka mataiafa ya Afrika tu ndio watakaoalikwa kusimamimi zoezi
hilo la Maoni ya katiba na uchaguzi uajao.
''Ispokuwa zile nchi ambazo sio adui wa Zimbabwe zitakaribishwa hapa,
ama nchi ambapo zimehusika katika kuiwekea Zimbabwe vikwazo vya aina yoyote
,hazitakuwa na ruhusa ya kuja kwenye uchaguzi na zoezi la kutoa maoni kuhusu
katiba ya Zimbabwe'' amsema wazei wa mambo yanje wa Zimbabwe
Mapema mwaka 2002 nchi za Maghari ikiwemo Marekani na Umoja wa uala EU
zilimuekea vikwazo vya kiuchumi Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pamoja na ofisa
mkuu wa chama chake cha Zanu P-F.
No comments:
Post a Comment