Language

Thursday, 10 January 2013

MICHEZO: TAIFA STARS YAWASILI ADDIS ABABA KUWAKABILI ETHIOPIA

Kikosi cha Taifa Stars.
TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefika salama Addis Ababa tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa kesho (Januari 11) katika Uwanja wa Addis Ababa kuanzia saa 11.30 jioni. Stars imefikia katika hoteli ya Hilton na itafanya mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Addis Ababa kwa saa moja kuanzia saa 11.30 jioni.
Imetolewa na:
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...