Wakali wa ngoma za Alingo na Beautiful Onyinye, Peter na Paul Okye
wanaounda kundi la P-Square, wametoa sababu inayowafanya wachukue muda
mrefu kutoa albamu mpya kuwa ni kukosekana kwa sapoti ya mama yao ambaye
alifariki dunia Julai 13 mwaka jana.

“Alipokuwa hai alikuwa ni sehemu ya mafanikio yetu hasa kipindi ambacho
tunaandaa albamu alikuwa akikesha nasi studio na kuombea hata kazi zetu lakini
sasa maisha yamekuwa magumu na sijui tutafanyaje albamu tutakapokuwa tayari
kuifanya”walilalamika wasanii hao.
Akifafanua zaidi Peter alisema kuwa mama yao alikuwa ni muumini mzuri
na alikuwa na kanisa lake ambalo walishirikiana kulijenga tunachofanya kumuenzi
ni kuhakikisha linaendelea.
No comments:
Post a Comment