KAMPUNI ya Compass Communications imewatahadharisha warembo na
wanamitindo wote nchini kutorubuniwa na genge la watu wanaotumia jina la
Flaviana Matata kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai
amesema jana kuwa kuna genge la watu wanaotumia ukurasa wa mtandao wa kijamii
wa facebook ujulikano kwa jina la Flaviana Matata’s na kujipatika fedha kiasi
cha sh. 200,000 kwa jila anayejiunga kwa lengo la kutafutiwa kazi au nafasi ya
kufanya shughuli za wanamitindo nje ya nchi.
Maria alisema kuwa watu hao huwarubuni wasichana na kuwaahidi
kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa mgongo wa Flaviana na mmoja wa vijana hao
amejitambulisha kama ‘kaka’ yake mwanamitindo huyo, jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa baada ya kukutana na wasichana waliongia katika mtego
huo, huwa wanaawalaghai kwa njia mablimbali na baadaye kulipa kiasi hicho cha
fedha. Alisema kuwa hali hiyo imewaletea usumbufu wasichana wengi na kujikuta
wakihaha kutafuta ukweli baada ya kutapeliwa.
“Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana
Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia yoyote
na ukurasa huu au watu hawa. Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe
waangalifu kwani Flaviana Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu
yoyote kazi ya uanamitindo popote pake,” alisema Maria.
Maria alisema kuwa ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa
Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” na kwa sasa wanendelea kushirikiana na
vyombo husika kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu huo.
No comments:
Post a Comment