Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoza machozi
kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama
makuu.
Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo
ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura
elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta.
Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu.
Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita
udanganyifu kwenye uchaguzi.
No comments:
Post a Comment