Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa
Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi
kadhaa, ikiwamo figo.Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi
zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya
kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili
kushindwa kufanya kazi.“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu,
lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua,
ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso,
alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga Khan lakini akasema kuwa
hadi jana jioni, hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri
No comments:
Post a Comment