Takriban wanajeshi 200 wa Nigeria wanatarajiwa
kuwasili nchini Mali kusaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji wa
kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
Ni kikosi cha kwanza cha jeshi kutoka Magharibi
mwa Afrika kujiunga na wanajeshi wa Ufaransa walioanza kupambana na
wapiganaji wa kiisilamu tangu Ijumaa iliyopita.
Jumla ya wanajeshi 3,300 wa kikanda
watapelekwa nchini Mali chini ya azimio la Baraza la Usalama la umoja wa
Mataifa. Chad imesema itapeleka wanajeshi 2,000.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wameanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya wapiganaji hao wa kiisilamu.
Duru zinasema kuwa makabiliano yalizuka kati ya
waasi na wanajeshi mjini Diabaly, umbali wa kilomita 350 kaskazini mwa
mji mkuu Bamako siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment